Na Tumsifu Kaoza
Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama
na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama
wangyama kazi. Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe na hutumika kama wanyama
kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili
ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale
wachache walioboreshwa.
Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika
makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya
maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na
ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-
i)
Kufuga ng’ombe katika eneo kwa
kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji
huria.
ii)
Kujenga banda au zizi bora.
iii)
Kuchagua koo/aina ya ng’ombe
kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
iv)
Kutunza makundi mbalimbali ya
ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
v)
Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana
na umri na mahitaji ya mwili.
vi)
Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama
inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
vii)
Kuvuna mifugo katika umri na uzito
muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
viii)
Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi
zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
ix)
Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na
matukio muhimu ya ufugaji.
MIFUMO YA UFUGAJI
Ng’ombe wanaweza kufugwa katika
mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi).
Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya
maji. Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa
kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho. Ufugaji wa shadidi
uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.
UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi
na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
- Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi
ya ng’ombe alionao.
- Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.
- Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
- Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila
mpangilio.
Matunzo mengine ya ng’ombe
yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya
ng’ombe husika.
BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE BANDA BORA
.
Band alijengwe sehemu ya mwinuko
mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
·
Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya
mvua, upepo, jua kali na baridi.
·
Kuta imara zenye matunda au
madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
·
Sakafu yenye mwinuko upande mmoja
ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
·
Lijengwe katika hali ya kuruhusu
kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo
ulioshindiliwa na kuweka malalo.
·
Paa lisilovuja na
Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika
ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa kuzingatia yafuatayo:-
·
Zizi likae mahali pa mwinuko
pasiporuhusu maji kutuama.
·
Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya
wezi na wanyama hatari.
·
Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na
umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
·
Zizi lifanyiwe usafi mara kwa
mara na
·
Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa
ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba,
eneo la kulishia na maji ya kunywa.
ZIZI BORA
Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko
isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa
zifuatazo:-
§ Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
§ Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
§ Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa
usafi mara kwa mara
§ Zizi la ndama liwe na paa ma
§ Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.
UCHAGUZI WA KOO NA AINA YA NG’OMBE
WA KUFUGA
Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji
anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe kwa kuzingatia malengo ya ufugaji
(nyama au maziwa).
NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili
ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa haraka na kuweka misuli mikubwa
iliyojengeka vizuri. Baadhi ya koo zenye sifa hizo ni pamoja na Boran,
Mpwapwa (nyama na maziwa), Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara
wao. Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano Ufipa,Gofo,
Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na chotara wao ndio hutumika
kama ng’ombe.
NG’OMBE WA MAZIWA.
Sifa za ng’ombe wa maziwa
zifuatazo:-
- Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea
kichwani.
- Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
- Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha
nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
- Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa
wastani
- Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
- Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa
kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.
Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa
kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental na
chotara watokanao na mchangoayiko wa aina hizo na Zebu.
UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA
NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI
UTUNZAJI WA NDAMA
Mfugaji anapaswa kutunza ndama
vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi
kuachishwa maziwa ni pamoja na
- Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia
maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto
(Tincute of Iodine) mara baada ya kuzaliwa na
- Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara
baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.
Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
Endapo jike aliyezaa amekufa au
hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a
mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
- Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
- Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia
joto la mwili.
- Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver
oili).
- Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
- Yai moja bichi
Koroga mchanganyiko huo, weka katika
chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa. Ndama anyweshwe
mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila mara
mchanganyiko uwe mpya. Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu ya
kidogo ili asipaliwe.
- Endapo ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama
anyweshwe maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
- Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama
ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1
- Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji
safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na
- Ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa
miezi 3. Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya
nzuri.
JEDWALI NA. 1 KIASI CHA MAZIWA NA
CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA
UMRI (WIKI)
|
KIASI CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA)
|
KIASI CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA
KWA SIKU (KILO)
|
1
|
3.0
|
0.0
|
2
|
3.5
|
0.0
|
3
|
4.0
|
0.0
|
4
|
4.5
|
0.0
|
5
|
5.0
|
0.1
|
6
|
5.0
|
0.2
|
7
|
5.0
|
0.3
|
8
|
4.0
|
0.4
|
9
|
3.0
|
0.7
|
10
|
2.0
|
1.0
|
11
|
1.5
|
1.25
|
12 – 16
|
0.75
|
1.5
|
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama
visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.
Matunzo mengine ya ndani ni pamoja
na:-
- Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara
zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
- Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike
- Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao
hawatahitajika kwa ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya
kuendelea kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
- Kuweka alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza
na ya tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa
udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
- Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
Huduma hizi zifanyike chini ya
maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA
KUACHISHWA MAZIWA HADI KUPEVUKA (MIEZI – 18)
- Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na
chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea umri wake na
- Ndama wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa
kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi.
UTUNZAJI WA MTAMBA
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha
umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza.
Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la ng’ombe. Miezi 3
kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-
- Malisho bora
- Maji ya kutosha
- Madini mchanganyiko na
- Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili
kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe
wenye mimba, wanaokamuliwa na madume. Mfugaji anapaswa kutunza vizuri
ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia malisho bora na maji safi ya kutosha
kila siku. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe wakubwa
ni pamoja na:-
- Ng’ombe apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10
au majani mabichi kilo 40 kwa siku kutegemeana na uzito. Iwapo malisho
hayatoshi hususan wakati wa kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na
mashambani) kama molasisi, mabua, maharage, mpunga n.k
- Ng’ombe apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini
mchanganyiko, unga wa mifupa na chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha
uzalishaji na
- Ng’ombe apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na
ushauri wa mtaalam wa mifugo.
UPANDISHAJI
Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe
kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha
anapata ndama bora na maziwa mengi. Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja
na
- Mtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 -24 na
uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito
wa kilo 200 kwa ng’ombe wa asili. (Rejea jedwali Na 2)
- Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na
- Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama
ana dalili za joto ili apandishwe tena. Iwapo ng’ombe ataendelea
kuonyesha dalili za joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri
wa mtaalam wa mifugo.
JEDWALI NA.2. UMRI NA UZITO
UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
AINA YA
NG’OMBE
|
UZITO
(KG)
|
UMRI
(MIEZI)
|
Friesian
|
240 – 300
|
18 – 24
|
Ayrshire
|
230 – 300
|
17 – 24
|
Jersey
|
200- 250
|
18 – 20
|
Mpwapwa
|
200 – 250
|
18 – 20
|
Chotara
|
230 – 250
|
18 – 24
|
Boran
|
200 – 250
|
24 - 36
|
Zebu
|
200
|
30 -36
|
DALILI ZA NG’OMBE ANAYEHITAJI
KUPANDWA
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili
za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa wakati. Dalili
hizo ni pamoja na
§ Kupiga kelele mara kwa mara
§ Kutotulia/kuhangaika
§ Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni
§ Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake na
§ Kunusanusa ng’ombe wengine
Ng’ombe akionyesha dalili za joto
apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa
mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni
apandishwe asubuhi).
UHIMILISHAJI
Uhimilishaji ni njia ya kupandikiza
mbegu kwa ng’ombe jike kwa kutumia mrija. Faida za uhimilishaji ni pamoja
na kusambaza mbegu bora kwa haraka na kwa gharama nafuu, kupunguza gharama za
kutunza dume na kudhibiti magonjwa ya uzazi.
ILI MFUGAJI ANUFAIKE NA HUDUMA HII
ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO:-
- Kuchunguza kwa makini ng’ombe mwenye dalili za joto
- Kumjulisha mtaalam wa uhimilishaji mapema ili kuwezesha
zoezi hili kufanyika kwa wakati.
- Kuchunguza kama ng’ombe atarudi kwenye joto siku ya 18 – 23
baada ya kupandishwa na
- Ng’ombe aliyepandishwa apimwe mimba siku 60 hadi 90 baada ya
kupandishwa.
MATUNZO YA NG’OMBE MWENYE MIMBA
Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi
9 hadi kuzaa. Katika kipindi hicho chote anastahili kupatiwa lishe bora
na maji ya kutosha ili akidhi mahitaji ya ndani aliye tumboni na kutoa maziwa
mengi baada ya kuzaa.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na
- Ng’ombe apewe lishe bora na maji ya kutosha kipindi
chote cha mimba
- Miezi 2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa
siku
- Apewe kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa
- Ng’ombe anayekaribia kuzaa, hususani mtamba, azoeshwe
kuingia kwenye sehemu ya kukamulia.
DALILI ZA NG’OMBE ANAYEKARIBIA KUZAA
Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za
ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze kufanya maandalizi muhimu. Dalili
hizo ni pamoja na
Kujitenda kutoka kwa wenzake
Kiwele kuongezeka
Chuchu kutoa maziwa zikikamuliwa
Kutokwa na ute mwekundu na sehemu za uke kuvimba na kulegea
Kuhangaika kulala chini na kusimama na
Kati ya saa moja hadi mbili kabla ya kuzaa sehemu ya uke
hutokwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha njia ya ndama kupita.
HUDUMA KWA NG’OMBE ANAYEZAA
Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi
wa karibu ili kuhakikisha usalama wa ng’ombe na ndama anaezaliwa. Mambo
ya kuzingatia ni pamoja na yafuatayo:-
- Sehemu ya kuzalia ng’ombe iandaliwe kwa kuwekwa nyasi
kavu na laini na iwe safi.
- Ng’ombe ahamishwe sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa
mara baada ya dalili za kuzaa kuonekana na
- Ng’ombe aachwe azae mwenyewe bifa usumbufu
MFUGAJI APATE USHAURI/HUDUMA KUTOKA
KWA MTAALAM IWAPO MATATIZO YAFUATAYO YATAJITOKEZA:-
- Ng’ombe kushindwa kuzaa kwa masaa mawili hadi matatu
baada ya chupa kupasuka
- Kondo la nyuma kushindwa kutoka masaa sita baada ya kuzaa
- Kizazi kutoka nje na
- Ng’ombe kushindwa kusimama baada ya kuzaa
MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA
Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji
kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa
maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe
v Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita
2 – 3 za maziwa anayotoa.
v Apewe madini na virutubisho vingine kulingan ana mahitaji
v Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza
maziwa.
v Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji
huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe.
v Baada ya kusitisha kukamuliwa apewe kilo 2 za chakula cha
ziada kwa siku hadi atakapozaa na
v Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba
kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
UZALISHAJI WA MAZIWA
Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa
maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazao yatokanayo na
maziwa .
Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
- Sehemu ya kukkamulia iwe safi na yenye utulivu
- Ng’ombe awe na afya nzuri msafi na kiwele kioshwe kwa maji
safi ya uvuguvugu.
- Mkamuaji awe msafi kucha fupi na asiwe na magonjwa ya
kuambukiza
- Inashauriwa mkamuaji asibadilishwebadilishwe
- Vyombo vya kukamulia viwe safi
- Muda wa kukamua usibadilishwe na
- Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo
maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
UCHAGUZI WA UTUNZAJI WA DUME BORA LA
MBEGU
Dume ndilo linalojenga ubora wa
kundi la ng’ombe katika masuala ya uzalishaji kutokana na uwezo wake wa
kupanda majike 20 – 25 wakati wa msimu wa uzalianaji (breeding season).
Ili kundi la ng’ombe liwe bora,
mambo yafuatayo yazingatiwe
§ Chagua dume kutoka kwenye ukoo ulio bora kwa kuzingatia
kumbukubu za uzalishaji wa maziwa au nyama za wazazi wake
§ Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua
dume bora
§ Lisha dume malisho bora na maji safi ya kutosha. Pia
apatiwe chakula cha ziada.
§ Katika ufugaji shadidi dume la ng’ombe lifugwe kwenye
banda imara lenye sehemu za kuwekea chakula maji na kufanyia mazoezi.
§ Katika ufugaji huria dume atengewe sehemu na kupatiwa
chakula cha ziada.
§ Dume livalishwe pete puani kwa ajili ya kupunguza ukali na
kuwezesha urahisi wa kumshika.
§ Dume apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingan ana ushauri
wa mtaalam wa mifugo na
§ Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua
dume bora.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe wengi wanaofugwa hapa nchini
Tanzania ni wa asili ambao kwa kiwango kikubwa hutumika kwa ajili ya uzalishaji
wa nyama. Hata hivyo uzalishaji wake wa nyama ni mdogo kutokana na kasi
ndogo ya kukua na kuwa na uzito mdogo wakati wanapopevuka. Hali hii
husababishwa na matunzo duni, kwa kuwa huchungwa/hulishwa kwa kutegemea malisho
peke yake ambayo hayawezi kukidhi mahitaji ya viinilishe vinavyohitajika kwa
ng’ombe.
Ili kuongeza kasi ya ukuaji na
kuongeza uzalishaji wa nyama, mfugaji anapaswa kufanya mambo yafuatayo:-
UTUNZAJI WA NDAMA
- Wajengewe banda/boma imara safi na lisilo na
unyevunyevu ili kuepukana na magonjwa kama kichomi na kuhara
- Waruhusiwe kunyonya kwa muda usiopungua miezi sita, pia
wapatiwe majani laini kuanzia wanapofikia umri wa wiki mbili ili waanze kula
mapema.
- Wapatiwe maji safi na yakutosha
- Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza
kizazi wahasiwe wakiwa na umri wa wiki mbili ili waanze kula mapema.
- Wapatiwe maji safi na yakutosha
- Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza
kizazi wahasiwe wakiwa na umri usiozidi miezi 3 ili wakue haraka na kuwa na
nyama nzuri.
- Wawekwe alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza
na ya tano kwa ndama wote, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio, kwa ajili ya
urahisi wa udhibiti wa umiliki na utunzaji kumbukumbu.
- Ndama wachungwe eneo tofauti na ng’ombe wakubwa kuepuka
maambukizi ya minyoo na magonjwa na
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA
KUACHISHWA KUNYONYA HADI KUPEVUKA (MIEZI 6 – 24).
Ndama wa umri huu anatakiwa apatiwe
- Malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote
- Vyakula vya ziada ili kukidhi mahitaji ya mwili (mifano ya
vyakula mchanganyiko imeonyeshwa kwenye jedwali Na. 3 ) na
- Tiba na kinga dhidi ya magonjwa hususan kinga ya kutupa
mimba (S19) kwa ndama jike watakaotumika kuendeleza kundi.
Katika kipindi cha miezi 6 hadi 24
mfugaji anashauriwa kuchagua ndama watakaoingizwa katika kundi la wazazi na
wanaobaki wawe katika kunenepesha kwa ajili ya nyama.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
Ø Apatiwe malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote
Ø Vyakula vya ziada (mifano ya vyakula mchanganyiko
iliyooneshwa kwenye jedwali Na.3), ili kukidhi mahitaji ya mwili.
Ø Vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 2 kila siku miezi
2 kabla ya kuzaa.
Ø Nafasi ya kunyonyesha ndama kwa miezi 6 mfululizo,
Ø Tiba na kinga dhidi ya magonjwa na
Ø Apandishwe kwa kutumia dume bora au kwa kutumia njia ya
uhimilishaji siku 60 baada ya kuaa.
UNENEPESHAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe kwa ajili ya nyama anaweza
kuchinjwa akiwa na umri wa kuanzia miezi 3 kulingana na mahitaji ya soko.
Kwa kawaida hapa Tanzania ng’ombe huchinjwa wakiwa na umri wa kuanzia miezi 18
kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya miezi 36 kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya
miezi 36 kwa ng’ombe wa asili.
Ili mfugaji aweze kupata faida
kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa nyama anapaswa afanye yafuatayo:-
- Afuge aina ya ng’ombe wanaokua na kukomaa haraka
- Anenepeshe ng’ombe kwa muda wa miezi 3 – 6 kabla ya
kuchinjwa. Unenepeshaji huongeza ubora wa nyama na kipato kwa mfugaji.
- Awapatie chakula chenye mchanganyiko wenye viinilishe vya
kutosha viinilishe vya kutia nguvu na joto mwilini viwe na uwiano mkubwa kuliko
vingine (Jedwali Na.3), na
- Auze ng’ombe mara wanapofikisha umri na uzito unaohitajika
katika soko ili kuepuka gharama za ziada.
JEDWALI NA.3. MFANO WA MCHANGANYIKO
WA CHAKULA KWA AJILI YA UNENEPESHAJI
AINA YA
CHAKULA
|
KIASI
KWA KILO
|
Majani makavu ya mpunga/NganoHey
|
23.3
|
Molasis
|
44.72
|
Mahindi yaliyorazwa
|
18.94
|
Mashudu ya Alizeti/pamba
|
11.4
|
Madini mchanganyiko
|
0.7
|
Chumvi
|
0.47
|
Urea
|
0.47
|
Jumla
|
100
|
UZALISHAJI NA UHIFADHI WA MALISHO
BORA NA VYAKULA VYA ZIADA
Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi,
vyakula vingine ni pamoja na miti malisho, mikunde na mabaki ya mazao.
Ili kupata malisho misimu yote ya mwaka ni muhimu kuvuna na kuhifadhi malisho
kipindi yanapopatikana kwa wingi. Inawezekana kupanda malisho mengi
kuliko kiasi kinachohitajika msimu mmoja/wakati wa mvua, kuyavuna yanapofikia
hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi (mfano wa malisho yanayoweza kupandwa ni
mabingobingo, Guatemala, African fox-tail, desmodium, centrosema, lukina
n.k). Malisho yakupandwa ni vizuri yawe na mchanganyiko wa jamii ya
nyasi, mikunde na miti malisho.
MASALIA YA MAZAO SHAMBANI
Masalia ya mazao shambani kama vile
mabua, magunzi, majani ya mikunde, viazi, ndizi, mpunga, na mengineyo yanaweza
kukusanywa na kuhifadhiwa vizuri kama chakula cha ng’ombe.
MALISHO YA MITI NA MATUNDA YAKE
Malisho yatokanayo na miti ya
malisho na matunda yake yanaweza kutumika kama malisho ya ng’ombe. Majani
na matunda ya miti ya lukina, sesibania, migunga na mbaazi yanaweza kukaushwa
na kuhifadhiwa kwa ajili ya kulisha ng’ombe.
VYAKULA VYA ZIADA
Ili kukidhi mahitaji ya viinilishwe
kulingana na kiwango cha uzalishaji, ng’ombe anatakiwa kupewa vyakula vya ziada.
Vyakula hivyo vinatokana na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali.
Michanganyiko hii inategemeana na upatikanaji wa malighafi katika maeneo
husika. Mifano ya mchanganyiko huo ni kama ifuatavyo:-
JEDWALI NA. 4 MFANO WA KWANZA WA
CHAKULA CHA ZIADA
AINA YA
CHAKULA
|
KIASI
(KILO)
|
Pumba za mahindi
|
47
|
Mahindi yaliyoparazwa
|
20
|
Mashudu ya alizeti/pamba
|
20
|
Unga wa lukina
|
10
|
Chokaa ya mifugo
|
2
|
Chumvi
|
1
|
Jumla
|
00
|
Mfano wa pili wa chakula cha ziada
ni tofali la kulamba lenye urea ambalo mchanganyiko wake ni:-
Unga wa mahindi
kilo 1
Pumba za
mahindi
kilo 3
Urea
kilo 1
Mashudu ya alizeti
kilo 2
Chumvi ya
kawaida
gramu 200
Unga wa mifupa
gramu 200
Chokaa ya
mifugo
kilo 1.5
saruji
kilo 1
mfugaji anatakiwa kuzingatia
yafuatayo ili kupata tija katika ufugaji:-
- kulisha mchanganyiko wa nyasi, mikunde na mchanganyiko wa
madini na vitamin
- kutenga maeneo kwa ajili ya kulisha ng’ombe kwa mzunguko
pamoja na kupanda malisho katika mfumo huria na nusu huria na
- kuvuna nyasi na mikunde inapofikia hatua ya kutoa maua na
kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa uhaba wa malisho hususan wakati wa kiangazi.
NJIA ZA KUHIFADHI MALISHO
Malisho yanaweza kuhifadhiwa kwa
kuyakausha (Hei) au kuyavundika (Sileji).
HEI
Hei ni majani yaliyohifadhiwa kwa
kukaushwa baada ya kukatwa au kuachwa kukauka yakiwa shambani kwa matumizi ya
baadaye. Katika kutengeneza hei yafuatayo yazingatiwe:-
- vuana malisho yanapoanza kutoa maua
- Yaanikwe kwa siku 3 hadi 6 kutegemea aina ya malisho na hali
ya hewa na yageuze mara 1 au 2 kwa siku ili yakauke vizuri.
- Yafungwe katika marobota baada ya kukauka inawezekana
kutumia kasha la mbao lenye vipimo vifuatavyo:- Urefu sentimeta 75, upana
sentimeta 45 na kina sentimeta 35 au mashine na zana za kufunga marobota ya hei
na
- Hifadhi marobota juu ya kichanja ili kuzuia maji yasiingie
unyevu na kuharibiwa na wadudu.
SILEJI
Sileji ni majani yaliyokatwakatwa na
kuvundikwa. Madhumuni ya kuyavundika ni kuyawezesha kubaki na ubora wake
hadi wakati yatakapotumika katika kutengeneza sileji yafuatayo yazingatiwe:-
v Tengeneza sileji kwa kutumia majani yenye sukari nyingi kama
mahindi au mabingobingo na mikunde, mabaki ya viwandani kama molasis,
v Andaa shimo au mfuko wa plastiki kulingana na kiasi cha
majani yaliyovunwa.
v Vuna majani ya kuvundika katika umri wa kuanza kutoa
maua. Endapo majani yaliyovunwa ni teketeke yaachwe kwa siku moja
yanyauke kupunguza kiwango cha maji.
v Katakata majani uliyovuna katika vipande vidogovidogo,
v Tandaza majani uliyokatakata ndani ya shimo au mfuko katika
tabaka nyembamba na kushindilia ili kuondoa hewa yote.
v Funika shimo ulilojaza majani kwa plastiki ikifuatiwa na
udongo.
v Sileji itakuwa tayari kutumika kuanzia siku 21 na
v Sileji iliyofunguliwa kwa ajili ya matumizi ifunikwe haraka
iwezekanavyo ili kuzuia kuharibika.
Sileji inaweza kubaki na ubora katika
shimo kwa muda mrefu kama haitafunguliwa na kuachwa wazi kwa muda mrefu.
UDHIBITI WA MAGONJWA YA NG’OMBE
Magonjwa huweza kusababishwa na
matunzo hafifu lishe duni na visababishi vya magonjwa kama vile protozoa
bacteria.
Virusi, riketsia na minyoo.
Aidha wadudu kama kupe na mbung’o wanasambaza visababishi vya magonjwa.
Afya bora ya ng’ombe inatokana na
kuzingatia mambo yafuatayo:-
Ndama apate maziwa ya awali (dang’a) ya kutosha kwa siku 3 –
4 baada ya kuzaliwa ili kuongeza kinga ya magonjwa mwilini.
Chovya kitovu cha ndama ndani ya madini joto (Tincture of
Iodine) mara baada ya kuzaliwa kuzuia kuvimba kitovu kutokauka au kutohudumiwa
ipasavyo mara baada ya ndama kuzaliwa. Kitovu huvimba na kutoa usaha
hukojoakwa shida na wakati mwingine huvimba viungo.
Ndama apewe dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 kama
atakavyoshauri mtaalam wa mifugo. Minyoo huwashambulia ndama zaidi hasa
wale walioana kula majani.
Zingatia usafi wa vyombo na band a epuka kumpa ndama maziwa
yaliyopoa na machafu ili kuzuia kuharisha.
Zingatia ujenzi wa mabanda kuruhusu mzunguko wa hewa ili
kuzuia ndama kupata ugonjwa wa vichomi. Vichomi huwapata ndama wa umri wa
miezi 5 au zaidi wanaofugwa ndani katika mabanda machafu yasiyo na mzunguko wa
hewa ya kutosha.
Ogesha ng’ombe kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo ili
kuua kupe wote wanaoleta magonjwa yatokana yo na kupe (ndigana kali na baridi,
kukojoa damu na maji moyo) na mbung’o (ndorobo) na
Ng’ombe wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali chanjo
muhimu ni za ugonjwa wa kutupa mimba, kimeta, ugonjwa wa miguu na midomo na
chambavu.
Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa
kwa mtaalam wa mifugo anapoona ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-
Ø Joto kali la mwili na manyonya kusimama
Ø Amepunguza hamu ya kula
Ø Amezubaa na kutoa machozi
Ø Anasimama kwa shind ana kusinzia
Ø Anapumua kwa shida na pua kukauka
Ø Anatokwa na kamasi nyingi
Ø Anajitenga na kundi
Ø Anaconda na
Ø Anapunguza utoaji wa maziwa ghafla
KUMBUKUMBU NA TAKWIMU MUHIMU
Kumbukumbu ni taarifa au maelezo
sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote
zinazohusiana na ufugaji. Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na
takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa ng’ombe. Kumbukumbu
zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu
mifugo husika na mifugo husika na mazao yake. Aidha humwezesha kuweka
mipango ya shughuli zake. Mfugaji anapaswa kuweka kumbukumbu muhimu
zifuatazo:-
§ Uzazi (uhimilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa,
kuzaa kuachisha kunyonya)
§ Kinga na tiba
§ Utoaji wa maziwa
§ Ukuaji
§ Idadi ya ng’ombe kwa makundi – majike, ndama, mitamba,
madume,maksai.