advert

advert

Wednesday, June 26, 2013


                                 
                          Nilikuwa napata utaalam wa kilimo hapa


                 Mzee Mwakibolwa akiwa katika shamba lake la nyumbani.


                        kilimo cha nyumbani hicho.


                                            



                                 Stella Mwaikusa
               
                       Mbegu bora chanzo cha uzalishaji wenye tija.

Mtaalam wa masuala  ya mbegu ambaye sasa ni msataafu Mica Mwakibolwa mkazi wa mbweni jijini Dar es salaam, anasema utaratibu wa mawakala wa mbegu ambao si wataalam wa kilimo, unawakatisha  tamaa wakulima, kwani  baadhi ya mawakala wamekuwa wakijali zaidi biashara kuliko nia sahihi ya kuwafanya wakulima wapate kile kinachohitajika.

Anasema pamoja na kuwepo kwa taasisi mbalimbali za utafiti wa mbegu bora, bado  utaratibu wa kufikisha mbegu hizo kwa wakulima ni tatizo linaloonekana kuwa sugu.

“Nafkiri suala la ufikishaji wa mbegu kwa mkulima  linatakiwa kusimamiwa na Serikali kwa ngazi zote pamoja na kuwa na bohari ya mbegu ya taifa” anashauri.
Mwakibolwa anaamini kuwa mbegu bora  ni chanzo cha uzalishaji wenye tija.

Sunday, June 23, 2013

 Mteja wa mihogo Dickens Mwakibolwa akiwa tayari ameshapata mihogo anayoihitaji na kuanza safari ya kuondoka shambani.
                                              shamba la mihogo la Paulo Masanja
                                           Mihogo ya ukweli! mitamu sana aisee.                       
                                Masanja akiwa anachimba mihogo tayari kwa kuiuza
                                       Du! hiyo mihogo ina unga kibaoooo
                                                      Jioneee mwenyewe, kilimo ni kila kitu bana!.
            Mteja wa mihogo Neema Mwaipopo akiwa tayari ameshahudumiwa



                         NANI AMEKWAMBIA DAR ES SALAAM HATULIMI?

 Masanja Paulo Mabula, ni kijana wa miaka  30 ambaye amepambana na maisha katika nyanja tofauti ili kuhakikisha anapata mkate wa kila siku, lakini hatimaye anajikuta katika maisha mengine kabisa ni baada ya kufanya kazi ya kuuza mchanga pale  ubungo, akaanza kazi ya ulinzi katika nyumba za watu, kupakia mizigo kwenye vituo vya daladala, hatimaye akagundua kuwa kilimo kinaweza kumfikisha mbali,  na ku jiingiza  kikamilifu katika kilimo cha mihogo.

Unaweza kufikiria labda haya yanazungumzwa ni kutoka mkoa fulani  ambako wengi tunaamini  ndiko kilimo kinakofanyika,  lakini amini usiamini haya yanafanyika katika jiji hili hili la Dar es salaam maeneo ya Mbweni wilaya ya Kinondoni.

"Nimenunua kiwanja kwa kazi hi ya kilimo, na nakuhakikishia mwaka huu hauishi nitakiwa nimeanza ujenzi wa nyumba yangu." anaeleza.

Utajiuliza Masanja ana shamba huko mbweni? jibu ni hapana, anachofanya ni kulima katika viwanja vya watu ambao bado hawajajenga kwa kile anachokiita kufanya usafi katika viwanja hivyo, kwa kulima mihogo ambayo inamletea kipato kikubwa zaidi kuliko kile cha kulinda viwanja hivyo.
Masanja anawashauri vijana waachane na mawazo ya kudharau kilimo kwani yeye anaamini kuwa kilimo ni fursa kubwa ya kufanikiwa.

"Unajua mtaji wa kilimo ni nguvu yako tu kwani mimi naandaa kila kitu mwenyewe na kwa siku nne tu nakuwa nimemaliza kusafisha shamba la heka moja." anasisitiza.