shamba la mihogo la Paulo Masanja
Mihogo ya ukweli! mitamu sana aisee.
Masanja akiwa anachimba mihogo tayari kwa kuiuza
Du! hiyo mihogo ina unga kibaoooo
Jioneee mwenyewe, kilimo ni kila kitu bana!.
Mteja wa mihogo Neema Mwaipopo akiwa tayari ameshahudumiwa
NANI AMEKWAMBIA DAR ES SALAAM HATULIMI?
Masanja Paulo Mabula, ni kijana wa miaka 30 ambaye amepambana na maisha katika nyanja tofauti ili kuhakikisha anapata mkate wa kila siku, lakini hatimaye anajikuta katika maisha mengine kabisa ni baada ya kufanya kazi ya kuuza mchanga pale ubungo, akaanza kazi ya ulinzi katika nyumba za watu, kupakia mizigo kwenye vituo vya daladala, hatimaye akagundua kuwa kilimo kinaweza kumfikisha mbali, na ku jiingiza kikamilifu katika kilimo cha mihogo.
Unaweza kufikiria labda haya yanazungumzwa ni kutoka mkoa fulani ambako wengi tunaamini ndiko kilimo kinakofanyika, lakini amini usiamini haya yanafanyika katika jiji hili hili la Dar es salaam maeneo ya Mbweni wilaya ya Kinondoni.
"Nimenunua kiwanja kwa kazi hi ya kilimo, na nakuhakikishia mwaka huu hauishi nitakiwa nimeanza ujenzi wa nyumba yangu." anaeleza.
Utajiuliza Masanja ana shamba huko mbweni? jibu ni hapana, anachofanya ni kulima katika viwanja vya watu ambao bado hawajajenga kwa kile anachokiita kufanya usafi katika viwanja hivyo, kwa kulima mihogo ambayo inamletea kipato kikubwa zaidi kuliko kile cha kulinda viwanja hivyo.
Masanja anawashauri vijana waachane na mawazo ya kudharau kilimo kwani yeye anaamini kuwa kilimo ni fursa kubwa ya kufanikiwa.
"Unajua mtaji wa kilimo ni nguvu yako tu kwani mimi naandaa kila kitu mwenyewe na kwa siku nne tu nakuwa nimemaliza kusafisha shamba la heka moja." anasisitiza.
Naam. Hakika kilimo ni fursa nzuri ya kujikwamua na umaskini. Akina Masanja ni wengi lakini hawajafikiwa ipasavyo kwa kuwa media zimewalenga sana wanasiasa. Hongera "Kilimo ni Fursa" kwa kuwakumbuka wajasiriamali kama hawa
ReplyDelete
Deleteumeona eee! tutafika tu