Stella Mwaikusa
UCHOMAJI
WA MASHAMBA KWA MAANDALIZI YA KILIMO
Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya
wakazi wa vijiji vya Luwe, Mkongo, nyaminywiri
wilayani Rufiji wamekuwa
wakichoma misitu kwa ajili ya kufukuza wanyama na kufanya maeneo hayo kuwa safi
na wakati mwingine wamekuwa wakiandaa mashamba kwa kuchoma moto kwa lengo
hilohilo la kusafisha.
Mara nyingi moto unaowashwa kwa
ajili shughuli hiyo hauishii sehemu
ambayo mhusika alikusudia kwani husambaa na kusababisha mazao mengine kama Miti
ya miembe, Mikorosho, migomba na kitu chochote kitakachokuwa karibu na mashamba au msitu basi kitapitiwa na moto
huo.
Nilipojaribu kumuuliza mkazi
mmoja wa kijiji cha nyaminywiri Said Mkumba aliniambia kuwa hiyo ni kawaida ya
baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kuchoma moto kila wanapoona msitu unakuwa
mkubwa na wengine wanaona raha tu wanapoona moto unawaka na kuenea maeneo
mbalimbali
“Huku kwetu ni jambo la kawaida
hasa kipindi cha kuandaa mashamba wakulima hutumia njia ya kuchoma moto
mashamba ili kuwarahishia kazi ya kutoa
majani” anaeleza saidi na kuongeza kuwa moto unapoenea na kuingia sehemu
isiyokusudiwa basi inaeleweka tu kuwa ni bahati mbaya.
No comments:
Post a Comment